-->

Afisa Muuguzi Daraja la II at TAMISEMI

Afisa Muuguzi Daraja la II.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) imepata kibali cha ajira mbadala chenye Kumb Na. FA 97/128/01/”A’’/31 cha tarehe 12 Julai 2019 kwa ajili ya kuajiri watumishi 550 wa kada mbalimbali za afya. Hivyo, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inapenda kuwatangazia wahitimu wote wa kada za Afya nchini kuwasilisha maombi ya nafasi za kazi, kuanzia leo tarehe 22/07/2019 ili kujaza nafasi mbalimbali za Kada ya Afya katika Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati.
Nafasi zinazotangazwa ni zifuatazo: – Afisa Muuguzi Daraja la II.

Waombaji wawe na Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo ya vitendo kazini (Internship) ya mwaka mmoja, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

SIFA ZA MWOMBAJI;
• Awe raia wa Tanzania;
• Awe na umri usiozidi miaka 45;
• Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au asiwe Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
• Asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini;
• Asiwe na check namba, na endapo itabainika kuwa aliwahi kuajiriwa Serikalini, atatakiwa kuzingatia utaratibu wa uhamisho au kurejea katika Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB 228/271/01 wa tarehe 07 Agost, 2012.

Job Skills: Not Specified
Job Education Requirements: Not Specified

MAOMBI YOTE YAAMBATANISHWE NA;
• Nakala ya cheti cha kidato cha nne/sita;
• Nakala za Vyeti vya Taaluma;
• Nakala ya cheti cha kuzaliwa;
• Nakala ya cheti cha usajili kamili (Full Registration) au Leseni ya kufanya kazi ya taaluma husika;
• Maelezo binafsi (CV); na
• Waombaji wanaojitolea na wale wanaomaliza muda wa ajira za mikataba kutoka kwa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Afya wanatakiwa kuambatanisha barua za uthibitisho kutoka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri husika.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE
• Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi Halmashauri yoyote watakayopangiwa;
• Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi na mashirika/taasisi zilizoingia ubia na Serikali;
• Waombaji waliosoma nje ya nchi wanatakiwa waambatanishe pamoja na equivalent certificate kutoka NECTA/NACTE/TCU; na
• Waombaji watakaotuma/waliotuma maombi yao ya kazi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto hawapaswi kuomba nafasi hizi za kazi za Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

How to Apply
  Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao (online) kupitia mfumo wa kielektroniki unaopatikana kupitia anuani ya ajira.tamisemi.go.tz. Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja Ofisini hayatafanyiwa kazi. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05 Agosti, 2019 saa 9:30 alasiri. Tangazo hili linapatikana katika tovuti yetu www.tamisemi.go.tz LIMETOLEWA NA: Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mji wa Serikali – Mtumba, S.L.P 1923, DODOMA. 22 Julai, 2019

You may like these posts