-->

Ajira Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Telegram “AFYA” DODOMA
Simu Na.255-26-2963341/2963342/2963346
 Nukushi: 255-26-2963348
Tovuti:www.moh.go.tz
(Barua zote ziandikwe kwa KATIBU MKUU)

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na. FA.97/128/01/”A”/31 cha tarehe12 Julai, 2019, inatangaza nafasi za kazi 163 za Kada mbalimbali za Afya kwa lengo la kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi katika maeneo yenye upungufu mkubwa wa wataalamu husika na hakutakuwa na kubadilisha pindi utakapopata nafasi hiyo.

Nafasi za kazi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-
1. Daktari Daraja la II (39)
2. Daktari wa Meno Daraja la II (6)
3. Mfamasia Daraja la II (4)
4. Afisa Afya Mazingira Daraja la II (2)
5. Afisa Muuguzi Daraja la II (11)
6. Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II (5)
7. Afisa Mteknolojia Daraja la II (Maabara) (3)
8. Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II (22)
9. Dobi (2)
10. Mfiziotherapia Daraja la II (3)
11. Mteknolojia Daraja la II (Dawa) (12)
12. Tabibu Daraja la II (9)
13. Mteknolojia Msaidizi (3)
14. Muuguzi Daraja la II (13)
15. Msaidizi wa Afya (29)

JUMLA 163
Sifa za Waombaji

1. Awe Raia wa Tanzania
2. Awe na Umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 45
3. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa na Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali, endapo Mwombaji alishaajiriwa Serikalini na kupata cheki namba, mwombaji atatakiwa kuzingatia Utaratibu wa Uhamisho au kurejea katika Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi ilivyobainishwa kwenye Waraka Na.CCB.228/271/01 wa tarehe 7 Agosti, 2012.

Mwombaji awe na sifa za Ueledi wa Mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba.1 wa mwaka 2009 kuhusu kada zilizo chini ya Wizara ya Afya.

Maombi yote yaambatanishwe na:-

1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa
2. Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne au/na cha Sita kulingana na Kada ya Mwombaji
3. Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts) na Wasifu (C.V)
4. Nakala ya cheti cha Usajili wa Taaluma Husika
5. Leseni ya kufanya kazi ya Taaluma husika
6. Picha ndogo (passport size) mbili za hivi karibuni

NB:

• Nakala za vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili
• Kwa waombaji watakaotuma maombi yao TAMISEMI hawapaswi kuomba nafasi hizi.
• Waombaji waliopo wanaojitolea katika Mikoa mbalimbali wapitishe maombi yao kwa Waganga Wafawidhi wa Mikoa husika. Mfano:-
Mganga Mfawidhi,

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke,
S.L.P ……….
DAR ES SALAAM.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta katika anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu (Afya),
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Ofisi Mpya za Mji wa Serikali – Mtumba,

S.L.P. 743,
DODOMA.
• Tangazo hili linapatikana kwenye tovuti ya Wizara:-
www.afya.go.tz
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 5/8/2019 saa 9:30 Alasiri.
Imetolewa na:
Gerard Julius Chami
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali – Afya
17/07/2019

You may like these posts