-->

Moto soko la Karume

 Moto soko la Karume

Soko la Karume lililopo Ilala jijini Dar es salaam, limeteketea kwa moto asubuhi ya leo Januari 16, 2022. Chanzo cha moto bado hakijajulikana. Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi.

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema baadhi ya maeneo katika Wilaya ya Ilala na Temeke yanakosa huduma ya umeme kutokana na moto uliounguza soko la Karume ambao umeathiri miundombinu ya umeme.

Tarifa iliyotolewa na shirika hilo leo Jumapili Januari 16,2022 kuhusu katizo la umeme la dharura imesema kuwa “Tunawataarifu wateja wetu wa Mikoa ya Ilala na Temeke kuwa, kutokana na ajali ya moto soko la Mchikichini Ilala, miundombinu ya umeme imeathirika kwa kuungua na kupelekea baadhi ya wateja wetu kukosa huduma ya umeme”.

Soko la Karume (soko la mchikichini) liliteketea moto usiku wa kuamkia leo na kuharibu mali mbalimbali ikiwamo miundombinu ya umeme.

Tanesco imetaja maeneo ambayo yataathirika katika Wilaya ya Ilala kuwa ni pamoja na; Kariakoo, Ilala sharifu shamba, Msimbazi Bondeni, mchikichini, Amana Hospitali,  Buguruni Malapa, Rozana, Kisiwani, Sokoni, Madenge, Banda la Ngozi, Msimbazi Centre, Utete, Pangani, lindi, Binti Kamba, Madenge Relini, Beriego,Alfukhan na maeneo ya jirani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maeneo yanayokosa huduma hiyo kwa upande wa Wilaya ya Temeke ni; Jamana, Chuma Road, Branket, Dakawa, Unubini, Maduka mawili, Keko toroli, Keko bora, Keko sigara, Temeke manispaa, Keko bora, Veta Changombe, Keko Magurumbasi, Msd,vKeko Mwanga, Keko juu, JKT Mgulani, Magereza, Jeshi la Wokovu, Uwanja wa Taifa wa ndani, Nyerere road, Tol gases, Jamana printers, Quality plaza, Toyota, Uniliver, Kiuta, Oilcom, mansoordaya, TTCL, Panasonic, King furniture, Gsm Pugu shopping Mall, superdol.

Pia, Tanesco imetaja meaneo mengine yanakayokosa umeme kwa upande wa Mbagala kuwa ni; Mission, Rangi tatu, Kimbangulile, Kiburugwa, Kingugi, kilungule, chamazi, charambe, saku, Majimatitu, Mzambarauni, Nzasa,serenge, Sabasaba, Kipati, Kibondemaji, Mwanagati, Kizuiani, Zakhiem na maeneo ya jirani.

Shirika hilo limesema kuwa jitihada zinaendelea za kuhakikisha huduma ya umeme inarejea mapema

“Mafundi wetu wanaendelea na jitihada za kuhakikisha huduma ya umeme inarejea mapema. Tunawaomba radhi wateja wetu kwa usumbufu unaojitokeza” imesema taarifa hiyo ya Tanesco

You may like these posts